NJIA ZA KUFANIKIWA KATIKA MAISHA

 Kila siku binadamu wote duniani tunajishughulisha ili tutimize malengo yetu, katika maisha kuna watu ambao wanafanikiwa katika mambo yao na kuna watu ambao hawafanikiwi. Binadamu tuna malengo na mahitaji katika maisha yetu, Malengo yanaweza yakawa ni masuala ya Elimu, Kazi, Ufundi, Cheo, Uongozi n. k

Tafiti zinaonesha ni watu wachache sana wanaotimiza malengo yao duniani kote inawezekana ukawa miongoni mwa watu ambao hawajafanikiwa kutimiza malengo yao, umehangaika sana kutimiza malengo yako lakini imeshindikana una muda mrefu sana unasaka maendeleo lakini unakosa, unakuta wenzako wanafanikiwa katika mambo yao wewe unashindwa.

Zifuatazo ni njia (9) bora zitazokufanya ufanikiwe katika maisha yako.

1.WEKA MALENGO YAKO.

Malengo ni dira, ni kitu pekee kinachokuonesha unahitaji kutimiza nini.Huwezi kufanikiwa wala kushindwa kama hujui unahitaji nini.

Kuna msemo unasema“Huwezi potea kama hujui unapokwenda “

Safari yoyote isiyo na mwelekeo basi kokote utakapoishia ni sawa tu.Malengo ni kipimo cha kushinda au kushindwa katika maisha yako.

Jiwekee malengo ya mwezi, miezi 3,miezi 6,mwaka au zaidi ya mwaka.Kwamfano unaweza kupanga kuwa na elimu ya kiwango fulani,kiongozi katika ngazi fulani au kumiliki biashara yako.Na pia malengo hayo yaambatane na muda.

Malengo yanakupa motisha ya kuendelea kusonga mbele na kutuonesha tumefanikisha jambo kwa kiasi fulani.

Wakati nilipokuwa shule ya sekondari nilikuwa na rafiki yangu ambaye yeye alikuwa anasoma sana na ni mtu ambaye alikuwa anajiwekea malengo yake ya kufaulu mtihani kwa kiwango cha juu sana kwenye masomo yake.Mimi pia nilikuwa nasoma sana lakini nilikuwa sijiwekei malengo ya namna gani nifaulu. Alikuwa ananishangaa sana tukifanya mitihani na kurudishiwa utakuta labda darasani yeye ndo kaongoza kwa kupata alama “A” ya 85% lakini utakuta analalamika kwamba amefeli, hakika ni jambo la kushangaza sana.

2.TENGENEZA MPANGO MKAKATI WA KUTIMIZA MALENGO YAKO.

Baada ya kujua unataka kutimiza malengo yako, nini na kwa muda gani unatakiwa upange ni jinsi gani unakwenda kutimiza lengo lako.

3.DHAMIRIA KUTIMIZA MALENGO YAKO (COMMITMENT ).

Hii ni sehemu muhimu sana ambayo kila mtafuta mafanikio anatakiwa kuwa nayo.Dhamira itakufanya kupigana kufa kupona ili jambo litimie, Moja ya sababu kubwa inayowafanya watu wengi washindwe kutimiza malengo yao ni kukosa dhamira ya dhati ya kutimiza malengo yao (lack of commitment).

4.KUWA TAYARI KUJITOA (HARDSHIP).

Kujitoa kunahitaji moyo uwe tayari kuyaacha mambo uliyoyazoea au unayopendelea kuyafanya na kuanza kufanya mambo yanayopelekea kutimiza malengo yako.

5.KUWA NA NIDHAMU NZURI.

Nidhamu ya kukamilisha malengo na hatua ulizojiwekea, kila jambo linahitaji nidhamu.

Nidhamu ni dhana muhimu sana ya kutumia wakati wa kusaka mafanikio ya aina yoyote ile.Hakuna mtu atakayekuja kukuforce wala kukusimamia katika kutekeleza mipango yako bali ni niwewe mwenyewe.

6.USIKATE TAMAA/NEVER GIVE UP.

Katika safari hii ya mafanikio huwa inakuwa na vikwazo vingi sana kwahiyo usikate tamaa songa mbele, muombe sana Mungu wako hata kama unapitia magumu kiasi gani we muombe Mungu tu, Mafanikio utayaona.

7.USIBWETEKE NA MACHACHE ULIYOANZA KUYATIMIZA.

Hapa ndipo wengi wanaposhindwa, katika safari ya mafanikio kuna vipindi.Kuna kipindi kitafika utaanza kuona matunda ya jitihada zako.

Watu wengi wakishaanza kuona matunda ya jitihada zao basi kama alikuwa anafanya kazi sana basi utakuta anaanza kuzembea katika kipindi ambacho unatakiwa ukazane tena sana yaani uongeze jitihada mara mbili yake.

8.WEKA BIDII SANA.

Katika kila jambo unalofanya lifanye kwa ufanisi mkubwa yaani wa hali ya juu, jitahidi kuweka bidii kwa kila jambo, Dunia ya sasa ni ya ushindani kila unachokifanya unatakiwa ukifanye kwa ufanisi mkubwa sana.Kila kitu ni kushindana ukifanya jambo kwa uvivu hautafanikiwa kamwe.

Waswahili wanakwambia “Mkono mtupu haulambwi “ , jitahidi sana uwe na kitu cha kukufanya uonekane ni mtu mashuhuri na si kingine bali kufanya unachofanya kwa bidii.

9.JITATHIMINI.

Kujitathimini ni kitu ambacho unatakiwa ufanye katika vipindi vyote vya kutimiza malengo yako.

Naamini kupitia njia hizi basi utakuwa mtu wa tofauti kabisa, natarajia nitaanza kukuona ukitimiza malengo yako na kukuona katika kilele cha mafanikio.

Post a Comment

0 Comments